Mkimkomalia Okwi, Kichuya anateleza kiulaini

Muktasari:

Simba wapo tayari jijini Mwanza na jana walikuwa uwanjani CCM Kirumba wakijifua kuwavaa Mbao FC kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu utakaopigwa leo Alhamisi.

Kocha Msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja amesema kuwa wachezaji wakewote wana uwezo wa kufunga mabao na kwamba ukimkaba Emmanuel Okwi basiShiza Kichuya atakufunga.

Simba wapo tayari jijini Mwanza na jana walikuwa uwanjani CCM Kirumba wakijifua kuwavaa Mbao FC kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu utakaopigwa leo Alhamisi.

Kocha Mayanja alisema kuwa vijana wake wapo fiti na wana uwezo wa
kufunga mabao, hivyo ukimkaba Okwi, basi ujue Kichuya au John Bocco
hawakuachi salama.

“Hatumtegemei mshambuliaji mmoja Okwi, ina maana ukimkaba huyo unampa
nafasi Kichuya kukumaliza, kwa hiyo mechi ya kesho lazima tushinde,”alisema Mayanja.