Wednesday, September 13, 2017

Mnigeria atibua mipango ya Njombe

 

By Gift Macha

Njombe. Kuchelewa kwa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) ya kiungo Mnigeria wa Njombe Mji, Ahmed Tajdin imetibua mipango ya kocha wa timu hiyo Hassan Banyai.

Tajdin amesajiliwa na Njombe ili kuipa makali safu ya kiungo ya timu hiyo lakini mpaka sasa bado hati yake hiyo haijawasili.

Mmoja ya viongozi wa Njombe maarufu kama Macho, alisema tayari wamefanya mawasiliano na Chama cha Soka Nigeria ili kupata hati hiyo.

Mwenyekiti wa Njombe, Erasto Mpete alisema tayari suala hilo linashughulikiwa ili kuweka mambo sawa.

Banyai alisema; "Ni miongoni mwa wachezaji tunaowategemea. Tunatamani apate ITC yake mapema.”

-->