Mohamed Ibrahim wa Simba afiwa na mtoto

Muktasari:

  • Mashabiki wa soka wamtumia salamu za pole wakimtia moyo awe mvumilivu katika kipindi hiki kigumu.

 Kiungo wa Simba, Mohamed Ibrahim ‘MO’ amefiwa na mtoto wake mchanga jana Jumanne katika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara aliandika kwenye ukurasa wake wa Istagram akimtakia pole kwa niaba ya uongozi wa klabu hiyo.

Alisema msiba huo wa mtoto mchanga umewaumiza watu wengi, hivyo akimsihi kuwa na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu.

Pia mchezaji mwenzake, Deus Kaseke alimtakia pole kwenye mtandao wa huo.