Mohamed Salah atwaa Tuzo ya Mchezaji Bora Afrika wa Mwaka BBC

Muktasari:

Wachezaji wenzake aliokuwa anashindana nao wampongeza kwa kuibuka kinara.

England. Shirika la Utangazi la Uingereza (BBC) limemzawadia mshambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah Tuzo ya Mchezaji Bora Afrika wa mwaka 2017.

Salah amewapiga kikumbo wachezaji wenzake Pierre-Emerick Aubameyang, Naby Keita, Sadio Mane na Victor Moses ambao walikuwa wanawania tuzo hiyo.

Mchezaji huyo tayari ametupia mabao 19 akiwa na Liverpool msimu huu. Baada ya kupokea tuzo hiyo ya BBC ya mchezaji bora wa mwaka alisema anafurahi kuwa mshindi wa tuzo hiyo na ni jambo la kipekee kwake kushinda.

Alisema ni matumaini yake ataongeza juhudi zaidi ikiwezekana ashinde tena tuzo hiyo mwakani.