Msanii wa filamu Bongo ajitwisha tifu la Zari v Diamond

Muktasari:

  • Hali hiyo ilisababisha sehemu ya kutoa komenti kuchafuka matusi kutoka upande wa mashabiki wa timu Hamisa ambayo imeanza kuja kwa kasi.

HUKU na Huku, tunaangukia kwa Shamsa Ford ambaye naye amefunguka juu ya ishu ya Diamond na Hamisa huku dizaini flani akimtupia dongo Hamisa.

Hali hiyo ilisababisha sehemu ya kutoa komenti kuchafuka matusi kutoka upande wa mashabiki wa timu Hamisa ambayo imeanza kuja kwa kasi.

“Adui wa mwanamke ni mwanamke mwenzie, haitakuja kutokea kamwe wanawake tukapendana, mwanamke ndo huwa mstari wa mbele kumzalilisha na kumuumiza mwanamke mwenzie. Kabla ya kumuumiza mwanamke mwenzio jaribu kuvaa viatu ingekuwa wewe ungefanyaje. Wanawake sisi dah tunahitaji maombi,” aliandika Shamsa Ford.

Aidha Shamsa alipotafutwa kujibu juu ya posti hiyo simu yake ilikuwa haipatikani na hivyo bado hali imebaki ya sintofahamu kwamba ameamua kuwa upande wa Zari lakini kwa alichoandika ni dhahiri yupo upande wa Zari lakini kwa matusi aliyopata ni noma sana.