Mtibwa Sugar yakumbatia wachezaji wake chipukizi, na kuwaachia nyota wake waondoke

Muktasari:

Kauli hiyo imetolewa na Afisa habari wa Mtibwa Sugar,  Thobias Kifaru amesema hawashangai wachezaji wao kwenda katika klabu za Simba na Yanga kwani kila mwaka hutokea jambo kama hilo na uzalisha vipaji wengine ambao watakuja kuwa tena tishio zaidi ya hao.

 Uongozi wa Mtibwa Sugar umesema hauna presha ya kuondokewa na wachezaji wake wa kikosi cha kwanza kwa sababu wanahadhina ya kutosha ya vijana.

Kauli hiyo imetolewa na Afisa habari wa Mtibwa Sugar,  Thobias Kifaru amesema hawashangai wachezaji wao kwenda katika klabu za Simba na Yanga kwani kila mwaka hutokea jambo kama hilo na uzalisha vipaji wengine ambao watakuja kuwa tena tishio zaidi ya hao.

"Sisi huwa atupendi kusajili wachezaji wakubwa na wenye majina ila huwa tunasajili wachezaji ambao hawana majina na hawajulikani na msimu huu tumewapandisha wachezaji watano kutoka timu ya vijana ambao tunaimani kuwa wanauwezo mkubwa wa kucheza ligi msimu ujao," anasema.

"Pia tunaendelea na mpango wetu ule ule wa kusajili wachezaji ambao hawajulikani kutoka katika timu za chini na hatuna mpango na wachezaji mbao wanamajina makubwa," anasema Kifaru.