Kibabage kuichezea Njombe Mji mzunguko wa pili

Muktasari:

Njombe ina mpango wa kusajili wachezaji wanne kwenye dirisha dogo, wawili ni hao kutoka Mtibwa Sugar  na wengine ni Wanyarwanda ambao muda wowote watasaini mikataba.

WACHEZAJI , Nickson Kibabage na Muhsin Malima wamejiunga na klabu ya Njombe Mji kwa ajili ya

mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara.

Njombe ambayo ina mpango wa kusajili wachezaji wanne kwenye dirisha dogo, wawili ni Kibabage na

Malima waliosajiliwa kwa mkopo kutoka Mtibwa Sugar  na wengine ni Wanyarwanda ambao muda wowote watasaini mikataba.

Kocha mkuu wa kikosi hicho, Mrage Kabange amesema, wachezaji hao wote wananne wanaendelea na mazoezi ndani ya kikosi chake kama kawaida.

"Mpango wetu ni kusajili wachezaji wanne kwenye dirisha dogo, wawili ni hao tumewaomba kwa mkopo kutoka Mtibwa  na wengine watakuwa ni hao Wanyarwanda kama mambo yatakwenda sawa,"anasema Kabange ambaye wakati timu nyingine zilipowaruhusu wachezaji wao kwenda mapumziko, yeye aliendelea nao kwa mazoezi.

Dirisha dogo la usajili lilifunguliwa rasmi Novemba 15 na linatarajiwa kufungwa Desemba 15.