Mwakyembe atoa neno la mwisho Lesotho

Muktasari:

  • Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dokta Harrison Mwakyembe ndiye kiongozi mkubwa kutoka Tanzania aliyeambatana na timu hapa Lesotho.

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dokta Harrison Mwakyembe amewataka wachezaji wa Stars kutambua dhamana waliyonayo saa chache kabla ya kuivaa Lesotho.

Stars na Lesotho zinacheza muda mfupi ujao kwenye Uwanja wa Taifa wa Lesotho jijini Maseru katika mchezo wa kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika mwakani.

Mchezo huo utachezwa mnamo saa 10 jioni kwa saa za hapa muda ambao ni sawa na saa 11 jioni kwa saa za Tanzania.

Waziri Mwakyembe amesema kuwa nyota wa Stars hawapaswi kuidharau Lesotho na badala yake wanapaswa kuhakikisha wanashinda mchezo wa leo.

"Nimewaambia wachezaji kuwa pamoja na wenyeji kuonekana kutokuwa na hamasa ya mchezo huu, hawapaswi kubweteka na badala yake wanatakiwa kujituma ili tuweze kushinda," alisema Waziri Mwakyembe