Mwanza Terminal waanzisha dozi Ndondo Cup

Muktasari:

  • Mchezo huo ulikuwa wa ufunguzi wa michuano hiyo, ambapo bingwa atajinyakulia kitita cha Sh3 milioni.

Mwanza. Mwanza Terminal imeanza vyema mashindano ya Ndondo Cup kwa kuichapa Buzuruga Terminal bao 1-0 katika mchezo uliopigwa jana Jumatano kwenye dimba la Nyamagana jijini Mwanza.

Mchezo huo ulikuwa wa ufunguzi wa michuano hiyo, ambapo bingwa atajinyakulia kitita cha Sh3 milioni.

Jumla ya timu 16 zilizogawanywa makundi manne zinapambana kusaka zawadi hiyo nono na leo mchezaji, Chika Chuku aliiwezesha timu yake hiyo kuipa ushindi kwa kufunga bao dakika ya 32 akiunganisha kona iliyochongwa na Ayoub Suleiman.

Mtanange huo ulionekana kuwa wa amshaamsha na ushindani kutokana na kila upande kuhitaji ushindi ili kujiweka nafasi nzuri.