Wenger atangaza kustaafu

Muktasari:

Kocha huyo amefundisha klabu hiyo kwa zaidi ya miaka 22

London, England. Kocha Arsene Wenger ametangaza kustaafu kuifundisha  Arsenal mwisho wa msimu huu baada ya kuiongoza klabu hiyo kwa miaka 22.

Mfaransa huyo ataondoka katika klabu hapo mwaka mmoja kabla ya kumalizika kwa mkataba wake wa sasa.

Gunners kwa sasa ipo nafasi ya sita katika msimamo wa Ligi Kuu na wanaweza kumaliza nje ya nne kwa msimu wa pili mfululizo, huku tumaini lao la kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa likiwa limebaki iwapo watachukua ubingwa wa Europa Ligi.

Wenger (68), ametwaa mataji matatu ya Ligi Kuu England na Kombe la FA mara saba huku akitwaa mataji mawili mara mbili kati ya mwaka 1998 na 2002.

"Nashukuru kupata nafasi ya kuifundisha klabu hii kwa miaka mingi yenye kumbukumbu," alisema Wenger. "Nimeiongoza klabu hii kwa kujitoa kwa moyo wangu wote na akili yangu.

"Kwa wote wanaopenda Arsenal, kuchukua jukumu la kulinda heshima ya klabu hii."

Mmiliki mkubwa wa Arsenal, Stan Kroenke alisema uamuzi huo wa leo Ijumaa kuwa "ni moja ya siku ngumu kwa wadau wa michezo baada ya miaka yote."

Aliongeza: "Mmoja ya sababu kuingia Arsenal tulikuwa tukitaka Arsene kuipa mafanikio klabu hii ndani na nje ya uwanja.