Nchimbi atoa onyo kali VPL

Muktasari:

Katika mechi zilizosalia kabla ya kumalizika kwa ligi, Njombe Mji itacheza na Ndanda, Singida United, Kagera Sugar, Mtibwa Sugar na Mwadui.

MSHAMBULIAJI wa Njombe Mji, Ditram Nchimbi amesema wamepanga kushinda michezo yao yote iliyosalia Ligi Kuu Bara ili kujinasua kwenye hatari ya kushuka daraja.

Njombe Mji inaburuza mkia kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 19 ilizokusanya katika michezo 25, kati ya michezo hiyo wameshinda tatu, sare 10 na kuchapwa mara 12.

“Hii ni hatari tupo kwenye nafasi mbaya ambayo kama tukizembea kidogo tu, tunashuka daraja lakini, mpango wetu ni kushinda mechi zilizobaki,” anasema mshambuliaji huyo.

Katika mechi zilizosalia kabla ya kumalizika kwa ligi, Njombe Mji itacheza na Ndanda, Singida United, Kagera Sugar, Mtibwa Sugar na Mwadui.