Neymar ataka kurudi Barcelona

Neymar.

Muktasari:

Kwa mujibu wa taarifa zilizofichuliwa na gazeti la Mundo Deportivo la nchini Hispania, mshambuliaji huyo ambaye kwa sasa anauguza mguu wake uliovunjika katika fainali za Kombe la Dunia amebadili mawazo na tayari ametuma ujumbe kuzungumza na uongozi wa Barcelona ili arudi badala ya kwenda Madrid.

Barcelona, Hispania. Wakati taarifa za nahodha wa Brazil, Neymar, kutakiwa na Real Madrid ya Hispania, zikizidi kuenea kila kona, siri imefichuka kuwa mshambuliaji huyo wa Paris Saint-Germain (PSG) ya Ufaransa anafanya mipango kimya kimya kurudi Barcelona.

Kwa mujibu wa taarifa zilizofichuliwa na gazeti la Mundo Deportivo la nchini Hispania, mshambuliaji huyo ambaye kwa sasa anauguza mguu wake uliovunjika katika fainali za Kombe la Dunia amebadili mawazo na tayari ametuma ujumbe kuzungumza na uongozi wa Barcelona ili arudi badala ya kwenda Madrid.

Neymar aliyeichezea Barcelona mechi 123 na kufunga mabao 68 kati yam waka 2013–2017,  aliushangaza ulimwengu alipoamua kuondoka Nou Camp na kwenda PSG kwa ada ya uhamisho ya Euro 222 milioni sawa na dola 264 milioni, lakini miezi saba baadaye anataka kurejea.

Katika uhamisho wake mengi yalisemwa baadhi wakiamini Neymar aliamua kukimbia mafanikio ya Lionel Messi ambayo yanamfunika mchezaji yeyote anayetua hapo, huku baadhi wakisema ulikua mpango wa Real Madrid, ambayo ilijitokeza na kubainisha nia ya kumsajili siku chache baadaye.

Madrid ilibainisha kuwa ipo tayari kumsajili Neymar kwa Euro 400 milioni, wiki iliyopita Kocha aliyeipa Real Madrid, taji la tatu mfululizo la Ligi ya Mabingwa Ulaya, Zinedine Zidane, ambaye kabla ya kubwaga manyanga, alikuwa kwenye harakati za kumsajili Neymar, alimfagulia akisema kutokana na ubora alio nao mshambuliaji huyo anahitajia na kila timu na anaweza kucheza kwenye klabu yoyote ile.