Wednesday, September 13, 2017

Njombe Mji wapiga maji ya Kandoro mazoezini

 

By Gift Macha

Huku Njombe hakuna mbwembwe na maisha yanakwenda poa tu. Wachezaji wa Njombe Mji wanapiga mazoezi makali halafu wanakunywa maji ya bomba kama kawa.

Timu hiyo inajifua kwenye Uwanja wa Chai kwa ajili ya mechi ijayo ya Ligi Kuu dhidi ya Mbeya City lakini kivutio kikubwa ni maji hayo wanayokunywa mazoezini.

Wakati Singida United ikipata udhamini wa maji ya kunywa kwa misimu miwili kutoka Kampuni Salim Bakhresa, hapa Njombe wanakomaa na maji ya bomba.

-->