Thursday, September 14, 2017

Okwi aanza kwa kishindo Ligi Kuu, abeba Tuzo ya Mchezaji Bora Agosti

 

By Doris Maliyaga

Straika wa Simba, Emmanuel Okwi raia wa Uganda ndiyo mchezaji bora wa Ligi Kuu bora Agosti mwaka 2017.

Okwi amechaguliwa mchezaji bora na kuwashinda, Mohamed Issa wa Mtibwa Sugar pamoja na Boniface Maganga wa Mbao FC.

Ni baada ya kufanya vizuri katika mechi yao ya kwanza walipoifunga Ruvu Shooting mabao 7-0, yeye akipachika manne na kuondoka na mpira wa hat-trick.

Mbali na ushindi huo, ameweka historia ya kufunga hat-trick ya kwanza msimu huu pamoja na mchezaji bora wa kwanza wa msimu huu. Amepata kitita cha Sh1mil zawadi ambayo hutolewa kwa kila mchezaji wa mwezi anayetangazwa kwa ubora.

Wachezaji alioshindwanishwa nao kwa upande wa Maganga, aliingia kwenye kinyang'anyiro hicho baada ya kufanya vizuri katika mechi yao ya ugenini walishinda kwa Kagera Sugar 1-0, ndiye alifunga.

Iko hivyo pia kwa Mohamed Issa ambaye alifunga bao pekee na kuipa ushindi timu yake iliposhinda kwa  Stand United 1-0 Manungu, Morogoro.

-->