Pambano la Mayweather vs Pacquiao

Muktasari:

  • Litavunja rekodi ya mapato duniani

Las Vegas, Marekani. Mazungumzo yamefikia mahali pazuri kwa kuhusu pambano la marudiano kati ya wababe wa uzani wa welter, Floyd Mayweather wa Marekani na Manny Pacquiao wa Ufilipino, likitarajiwa kupigwa Desemba mwaka huu.

Mabondia hao wameanza majadiliano kupitia kambi zao, ili kupata pambano la marudiano baaya lile la awali lililofanyika mwaka 2015 kumalizika kwa utata Mayweather akishinda kwa pointi huku Pacquiao akipinga ushindi huo, lakini pambano hilo linaweza kuvunja rekodi ya Dunia kwa mapato.

Mayweather, mwenye miaka 41, alitangaza kustaafu ngumi baada ya pambano hilo lakini alicheza tena mwaka jana dhidi ya Conor McGregor na kushinda hivyo kumfanya kushinda mapambano yake yote 50 aliyocheza ya ngumi za kulipwa.

Ili kumshawishi Pacquiao akubali kurejeana naye, Mayweather amependekeza alipwe fedha zaidi yake tofauti na ilivyokuwa mwaka 2015 ambapo yeye alilipwa Pauni 250 milioni.

Naye Pacquiao, mwenye miaka 39, anaonekana kufurahia kupata nafasi ya kurudiana na Mayweather akimini atamshinda kwani katika pambano lililipita lililofanyika Las Vegas alishindwa kwa pointi licha ya kupiga ngumi nyingi.