Pochettino pombe imempa msongo Lloris

Muktasari:

  • Ni baada ya kupigwa faini na kufungiwa kuendesha gari

London, England. Kocha wa Tottenham, Mauricio Pochettino, amesema anaamini maumivu ya msuli aliyoyapata kipa namba moja na nahodha wa timu hiyo, Hugo Lloris, yanatokana na msongo wa mawadho na maradhi ya afya ya akili.

Akifafanua alisema anaamini baada ya kipa huyo kuadhibiwa kutokana na kukamatwa akiendesha gari huku akiwa amelewa kumemsababishia mfadhaiko ambao sasa umeanza kumtesa.

Alisema kabla ya tukio hilo Lloris hakuwa mtu wa kuumia umia hivyo anadhani maumivu ya msuli yaliyomtu wiki iliyopita walipoichapa mabao 3-0 Manchester United yana uhusinao mkubwa na msongo wa mawazo uliomkumba.

Pochettino aliweka wazi kuwa kipa huyo anaweza kuendelea kuwa majeruhi kwa kipindi kirefu kijacho kutokana na kadhia hiyo ya msongo wa mawzo iliyosababishwa na nahodha huyo wa Ufaransa, kunywa pombe kupita kiasi wakati akijipongeza na wenzake kwa kutwaa Kombe la Dunia 2018.

“Bilas haka Lloris atakuwa kwenye msongo wa mawazo juu ya kilichomtokea hilo ndilo lililosababisha hata kupata maumivu ya msuli, ingawa kukaa kwake nje ni tatizo lakini ninahisi kama litasaidia kumuondolea mawazo,” alisema.

Lloris amepigwa marufuku ya kuendesha gari na faini Pauni 50,000 na Mahakama mjini London, kutokana na kurudia kosa la kuendesha gari huku amelewa katikati ya jiji hilo.