Kiwango cha Pogba chamnyima namba Ufaransa

Muktasari:

  • Kiungo huyo amepoteza namba ya kudumu katika kikosi cha kwanza cha Man United hivi karibuni

Kiungo wa Manchester United, Paul Pogba ameachwa katika kikosi cha Ufaransa kitakachoanza dhidi ya Colombia kutoka na kushuka kwa kiwango chake.

Ufaransa watakuwa nyumbani kwenye Uwanja wa Stade de France kuwakaribisha Colombia leo usiku kabla ya kwenda Russia kuwavaa wenyeji wa Kombe la Dunia hapo Machi 27.

Pogba atakuwa benchi kwa mechi ya tatu mfululizo ya Ufaransa ikiwa inajiandaa kwa Kombe la Dunia 2018, kwa mujibu wa taarifa kutoka Ufaransa.

Kiungo wa Manchester United (25), amecheza kwa dakika 30 katika michezo miwili iliyopita ya klabu yake dhidi ya Brighton na Sevilla.

Pamoja na Kocha wa Ufaransa, Didier Deschamps amekuwa akimtetea Pogba wakati wote, lakini gazeti la L’Equipe limeripoti kuwa kiungo huyo atakaa nje katika mchezo ujao ukokana na kushuka kiwango.

Kiungo wa Chelsea, N'Golo Kante atacheza pamoja na nyota wa Juventus, Blaise Matuidi, with Thomas Lemar na Kylian Mbappe katika mfumo wa 4-4-2.

Antoine Griezmann na Olivier Giroud watakuwa katika safu ya ushambuliaji na Deschamps anaweza kumtumia Mbappe kwa kushambulia ili kuwa na washambuliaji watatu.