Rasta wa Azam ampa salute Bocco

Muktasari:

  • Jana Bocco alifunga bao la kideoni katika mchezo wa Ligi Kuu ambao Simba iliibugiza Mwadui mabao 3-0.

Dar es Salaam. Beki wa Azam Yakubu Mohammed amemsifu mshambuliaji John Bocco na kumtakia maisha mema katika klabu yake ya Simba.

Jana Bocco alifunga bao la kideoni katika mchezo wa Ligi Kuu ambao Simba iliibugiza Mwadui mabao 3-0.

Yakubu alisema Bocco ni mpambanaji na anayeweza kutumia vizuri nafasi anazopata.

"Analijua goli muhimu viungo wa Simba wajue jinsi ya kumchezesha," alisema Yakubu ambaye alikuwepo uwanjani kushuhudia mchezo huo.