Rekodi yaiua Mwadui kwa Yanga

Muktasari:

Timu hizo zinakutana kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo Jumatano ikiwa ni mchezo wa Ligi Kuu.

Dar es Salaam. Timu za Yanga na Mwadui zinashuka leo kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam ikiwa ni mwendelezo wa mechi za Ligi Kuu.

Mchezo huo unatabiriwa kuwa mkali kuitokana na rekodi ya hivi karibuni kwa timu za mikoani kupambana ili kuhakikisha inazifunga timu vigogo.

Hata hivyo, rekodi bado inaonyesha Mwadui haijawahi kutoka sare na Yanga katika mechi zake walizokutana jijini Dar es Salaam.

Hivi sasa Mbao FC, Singida United ni miongoni mwa timu ambazo zimegeuka kuwa mwiba zinapokutana na timu vigogo kwenye Ligi Kuu.

Ushindi kwa Mwadui unaweza kuwaingiza kwenye historia ya kuwa miongoni mwa timu ambazo siyo za kubezwa.

Yanga inashuka kwenye mchezo huo ikiwa nafasi ya nne na pointi 21, huku Simba wakiwa  kileleni na pointi 26 ambapo wana tofauti ya tano na watani na watani zao.