Ronaldo aichoka Real

Tuesday November 14 2017

 

Madrid, Hispania .TAARIFA kambi ya Real Madrid zinasema Cristiano Ronaldo ameweka wazi msimamo wake wa kuondoka mwishoni mwa msimu huu.

 Habari ni kwamba mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United alimfuata Rais wa Real Madrid Florentino Perez na kumwambia wazi kwamba anaondoka.

Pia, imefahamika kwamba  Perez hayupo tayari kumruhusu mchezaji huyo aondoke na kwamba alimpa ofa mpya mezani, hata hivyo Ronaldo amekataa.

Imeelezwa kwamba Ronaldo hana furaha baada ya kuona  Real inatumia nguvu nyingi kutaka kumsajili  Kylian Mbappe kutoka Monaco na wiki hii kumekuwa na habari kwamba Real inamtaka kwa udi na uvumba nyota wa PSG Naymar.

  "Sitaki kuchukua mkataba mpya, nina amani na mkataba wangu wa sasa," Ronaldo aliliambia shirika moja la habari la Hispania.

 

Advertisement