Ronaldo asaini Juventus aota makubwa

Muktasari:

  • Mshambuliaji huyo wa Ureno mwenye miaka 33, amejiunga na mabingwa wa Italia Juventus kwa gharama ya pauni 99.2milioni baada ya kucheza kwa miaka tisa Real Madrid.

Turin, Italia. Cristiano Ronaldo amesema amekuwa mwenye bahati ya kutakiwa na Juventus, kwa kuwa wachezaji wa umri wake kwa kawaida wanakwenda Qatar au China.
Mshambuliaji huyo wa Ureno mwenye miaka 33, amejiunga na mabingwa wa Italia Juventus kwa gharama ya pauni 99.2milioni baada ya kucheza kwa miaka tisa Real Madrid.
"Kuja kucheza katika klabu kama hii, ni jambo la faraja kwangu," alizungumza wakati akitambulishwa Turin.
Ronaldo pia alisema kwake ni bahati kucheza katika timu ya Italia yenye lengo la kupata taji la Ligi ya Mabingwa.
Aliongeza kuwa halikuwa hajapata ofa yoyote kutoka sehemu nyingie.
Ronaldo amefunga mabao 450 akiwa na Real ametwaa mataji manne ya Ligi ya Mabingwa na makombe mawili ya La Liga tangu alipojiunga nao akitokea Manchester United mwaka 2009.
Mshindi mara tano wa Ballon D'Or pia, alitwaa ubingwa wa Uero 2016 akiwa na kikosi cha timu ya taifa ya Ureno.
"Nataka kushinda mataji," alisema. "Nataka kuwa bora yule mliyezoea kumuona, labda naweza kushinda tena Ballon d'Or, kila kitu kitatokea kwa wakati wake,” alisema Ronaldo.
Mamia ya mashabiki wa Juventus walijitokea kumpokea Ronaldo aliyewasili kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya afya asubuhi.
Mreno huyo aliwasili mjini Turin jana Jumapili akiwa  na ndege yake binafsi na leo asubuhi alifika J Medical Centre karibu na Uwanja wa Allianz kwa ajili ya vipimo hivyo.
Ronaldo alisaini jezi kwa mashabiki waliokuwa wakimsubiri na huku wakiimba jina lake.
Mmchana Ronaldo alikutana na kocha  Juventus, Massimiliano Allegri na wachezaji wenzake wapya.
Mashabiki wa Juventus walijitokeza nje ya hospitali tangu asubuhi kwa ajili ya kumuona shujaa wao mpya wakiwa na bango yao pamoja na jezi  'Ronaldo 7'.