Sesema ataboa siri ya kuishika Yanga

Muktasari:

Mwadui imefanikiwa kupata sare yake ya kwanza dhidi ya Yanga kwenye uwanja wa Uhuru

 Dar es Salaam. Kocha wa Mwadui, Ally Bizimungu amemuongezea ujuzi Abdallah Seseme baada ya kiungo huyo kumudu kucheza nafasi ya kiungo mkabaji na mshambuliaji katika kikosi hicho.

Sesema alifanikiwa kuwakaba vilivyo viungo wa Yanga katika mchezo uliomalizika kwa suluhu kwenye Uwanja wa Uhuru.

Seseme alisema ni kweli kocha huyo aliwataka wacheze yeye na Awadh Juma kwa kushambulia wote na kukaba kwa pamoja, baada ya kocha huyo kutambua uwezo wa viungo wa klabu ya Yanga.

“ Mwalimu katika mazoezi alikuwa anatuelekeza namna ya kucheza, hivyo tulichokifanya sisi ni kufuata maelekezo ya mwalimu, ndio maana nilikuwa nakaba,pia napiga pasi za kupeleka mashambulizi, tulitakiwa wote tufanye majukumu yote kwa pamoja, siyo kwamba Awadh akabe tu alafu mimi nishambulie,” alisema.

Kiwango cha kiungo huyu kimekuwa ni kiwango ambacho kinadumu na sio kushuka kama wengine, lakini alisema kitu bora alichonacho ni kutambua muda sahihi wa yeye kufanya nini na vitu gani anatakiwa asivifanye.

“Kikubwa mchezaji anatakiwa atambue nini anatakiwa kufanya na kwa wakati gani, muda ni jambo sahihi sana, mimi najitunza na bado najua kuwa sijafikia malengo yangu na hiyo ndiyo sili ya mimi kupambana kila siku,” alisema.