Thursday, September 14, 2017

Sharapova awajia juu wabaya wake

 

Marekani. Staa wa tenisi duniani, Maria Sharapova, ambaye alifungiwa mchezo huo kwa miezi 15 kutokana na kubainika kutumia dawa za kusisimua misuli, amewajia juu wanaomshutumu akisema hawana ushahidi huo.

  Mchezaji bora huyo wa zamani alikumbana na adhabu hiyo mwaka jana baada ya kukiri kutumia dawa zenye kemikali zilizokatazwa michezoni.      Alishutumniwa sana baadaye huku mchezaji mwenzake, Eugenie Bouchard, akipendekeza Sharapova asirejeshwe tena mashindanoni.

  Lakini sasa Sharapova anasema hakufanya udanganyifu wowote na anapuuzia mkasa huo.

“Nadhani shutuma zao hazina ushahidi, hivyo hazitatawala akili yangu.”

 

-->