Simba, Yanga, Mtibwa wapewa vibonde, waanzia nyumbani Kombe FA

Muktasari:

  • huu ni msimu wa nne wa Kombe la Azam Sports Federation Cup, mashindano ambayo hutoa timu ya kuiwakilisha Tanzania Bara kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.

Dar es Salaam. Droo ya raundi ya sita ya mashindano ya Azam Sports Federation Cup msimu huu imezipa mchekea timu za Yanga, Simba, mabingwa watetezi Mtibwa Sugar na  Azam ambazo licha ya kupangwa na vibonde, zitaanzia nyumbani.

Mabingwa wa kwanza wa taji hilo waliotwaa msimu wa 2015/2016, Yanga wataanzia nyumbani kwenye Uwanja wa Taifa jijini kukabiliana na mshindi wa mchezo baina ya Ihefu na Tukuyu Stars.

Ikumbukwe kuwa msimu uliopita, Yanga ilikutana na Ihefu FC katika hatua ya 16 bora ya mashindano hayo na kuibuka na ushindi wa penalti 4-3 jijini Mbeya.

Simba iliyotwaa ubingwa wa mashindano hayo msimu wa 2016/2017 na kisha msimu uliopita kuondolewa kwenye hatua ya 32 na Green Warriors iliyokuwa inashiriki Ligi Daraja la Pili kipindi hicho, nayo imepangwa kuanzia nyumbani dhidi ya Mashujaa FC kutoka mkoani Kigoma.

Mabingwa watetezi Mtibwa Sugar wenyewe watakuwa nyumbani Manungu Complex kuwakaribisha Kiluvya United.

Azam FC ambayo imekuwa na bahati mbaya kwenye mashindano hayo yenyewe pia itaanzia nyumbani kwenye uwanja wa Azam Complex jijini ambako itacheza dhidi ya mshindi wa mchezo baina ya Madini FC na Stand Babati.

Ratiba ya jumla ya mechi za hatua hiyo ambayo itachezwa kati ya Disemba 21, 22, 23 na 24 hii hapa ikijumuisha na namba ya mchezo husika.

55. Namungo vs Sahare/Deportivo

56. Geita Elect/ Kumuyange vs Kagera Sugar

57. Mtibwa vs Kiluvya United

58. Lipuli vs Laera/Mitumba

59. Stand United vs Ashanti United

60. Changanyikeni/Baga FC vs Coastal

61. Reha vs Zakhem/Mkamba Rangers

62. Majimaji vs Toto/gipco

63. Boma vs Njombe Mji

64. Pan Africa/ Villa Sqd vs Mwadui

65. Cosmo vs Green Warriors

66. Rhino vs Nyamongo/Bulyanhulu

67. Azam vs Madini/Stand Babati

68. KMC vs Prisons

69. Kili heroes/Forest vs Polisi tz

70. Majimaji R/moro kids vs Mbeya Kwanza

71. Geita gold vs Biashara United

72. R shooting vs Mucoba/might elephant

73. Yanga vs Ihefu/Tukuyu

74. Singida vs Arusha FC

75. Sharp striker/usalama vs Friends rangers

76. Dodoma vs Kasulu Stars/ home boys

77.  Mufindi United vs Alliance

78. Mbeya City vs Mgambo Shooting

79. African Lyon vs Arusha United

80. Simba vs Mashujaa fc

81. La familia /area c vs Mawenzi Market

82. Mbao vs Dar city

83. Milambo/Stand Dortmund vs JKT Tz

84. Mtwivila/Livingstone vs Pamba

85. Ndanda vs Transit Camp

86. Kitayosce/african sports vs Mlale fc