Simba hawajapoa, Kessy aliamsha

Muktasari:

Wakati wanaingia uwanjani mashabiki wa Simba waliokuwa uwanjani hapa walionekana hawajapoa kwani walipiga shangwe la maana

Beki wa kulia wa Nkana Rangers Kessy Ramadhani aliliamsha kabla ya mechi kuanza.
Ilikuwa hivi, wakati kikosi cha Nkana kinaingia kupasha misuli moto Kessy ambaye ni Mtanzania alikuwa wa pili kuingia na kufanya tukio la aina yake.
Kessy alipoingia uwanjani alikwenda moja kwa moja katika goli la Simba na kuingia ndani ya njavu huku akishika nyavu hizo.
Baada ya kumaliza tukio hilo Kessy wachezaji wengine baadhi wa Nkana walifanya tulio hilo la Kessy.
Pia wachezaji wa Simba wakati wanaingia kupasha misuli walifanya tukio la aina yake.
Ilikuwa hivi, wakati wachezaji hao wanaingia uwanjani kupasha misuli moto kabla ya mechi kuanza walizunguka mpaka kwenye kibendera cha kona goli la kusini ndio wakaingia uwanjani.
Wakati wanaingia uwanjani mashabiki wa Simba waliokuwa uwanjani hapa walionekana hawajapoa kwani walipiga shangwe la maana.
Shangwe ambalo walipiga mashabiki wa Simba waliwafunika wale wa Nkana ambao walifanya hivyo wakati timu yao inaingia uwanjani.