Omog Simba ndiyo basi tena

Muktasari:

  • Simba ilicheza mechi tofauti za kirafiki katika mikoa ya Mbeya na Rukwa

POINTI sita walizozipata Simba kutoka kwa Tanzania Prisons na Mbeya City zimemfanya kocha,  Joseph Omog atunishe misuli na akasisitiza, sasa ni mwenzo wa ushindi tu.

Simba ndiyo vinara wa ligi kuu, wanaongoza na pointi 22 ambazo ni sawa na Azam FC wanaoshika nafasi ya pili, wakati watani wao Yanga ni wa tatu na pointi 20.

"Ligi imekuwa ngumu kupita kiasi, lakini kwa upande wetu, tunasema kila mechi kwetu ni ushindi kuhakikisha hatung'oki kileleni,"alisema Omog.

Simba ambayo ikiwa katika michezo hiyo, ilifanya ziara ya kutembea katika Mkoa wa Rukwa na kucheza mechi tofauti za kirafiki.