VIDEO: Simba yaficha silaha zake Milford Lodge Zambia

Muktasari:

  • Mastaa Simba waishi kifahari Zambia

Kikosi cha Simba kimefikia katika hoteli ya The Milford Lodge iliyopo hapa Kitwe Zambia tangu jana Alhamisi.

Hoteli hiyo ambayo kwa siku unalipia Dola 100 kwa chumba kimoja ipo mahala kwenye utulivu na ukimya wa hali ya juu.

Mapema leo Mwanaspoti ilishuhudia nyota wa Simba wakipata chai katika ukumbi uliokuwa ndani ya hoteli hiyo.

Wachezaji wa Simba muda mwingi wamekuwa nadra kuonekana wakikatiza katika hoteli hii.

Muda mwingi wachezaji wote walionekana kujifungia vyumbani mwao huku umakini na utulivu ukiwa mkubwa ndani ya hoteli hii.