Simba yafunga mapema dirisha la usajili

Muktasari:

  • Ofisa Mtendaji mkuu wa C Magori amesema hakuna usajili ambao utafanywa na kikosi hiko katika dirisha dogo zaidi ya Zana Culibaly.

Dirisha dogo la usajili wa Ligi Kuu Bars litafungwa kesho Desemba 15 huku kila timu ikiweka wazi majembe yao mapya waliowaongeza katika na wale ambao wamewaacha.

Kikosi cha Simba ambacho kipo hapa nchini Zambia kupitia kwa Ofisa Mtendaji mkuu C Magori alisema hakuna usajili watakaoufanya tena.

Magori alisema usajili ambao wameufanya kwa Zana Colibaly ndio huyo huyo na hakuna mchezaji ambaye ataongezeka katika dirisha dogo.

"Tumemuongeza Colibaly kwani tulikuwa na shida upande wa mlinzi wa kulia baada ya kuumia kwa Shomary Kapombe, " alisema.

"Tulipanga kumuongeza straika kwani tulikuwa na ofa kutoka kwa timu nyingine kuwahitaji washambuliaji wetu lakini mpaka sasa nadhani halita wezekana kwa kipindi hiki, " alisema.

"Kwa maana hiyo hakutakuwa na usajili mwingine kwa kipindi hiki na wachezaji tuliokuwa nao wanaenea," alisema Magori.

Magori ndio mkuu wa msafara wa Simba uliokuwa hapa Kitwe Zambia.