Simba yamnasa kocha wa Mazembe

Muktasari:

  • Miamba hiyo ya Tanzania inasaka kocha mwingine wa kiwango cha juu baada ya kumtimua Joseph Omog

SIMBA inatarajia kufanya mabadiliko mengi kwenye benchi lake la ufundi baada ya kumleta kocha mpya, Hebert Velud kuhakikisha inaendelea kufanya kweli kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara kuubeba ubingwa ambao umekuwa ukiifukuzia kwa misimu kadhaa sasa.

Velud, ambaye ni Mfaransa ni kocha mwenye uzoefu wa soka la Afrika na kwamba atatua Msimbazi kuwa kocha mkuu baada ya vinara hao wa ligi kumfuta kazi Joseph Omog.

Kocha Velud, aliyezaliwa Juni 8, 1959 aliwahi kuzinoa Es Setif na USM Alger za Algeria, TP Mazembe za DR Congo na Etoile du Sahel ya Tunisia. Kocha huyo aliwasili jijini Dar es Salaam jana Jumapili.