VIDEO: Simba yapiga tizi ufundi mwingi Jumapili hapatoshi

Muktasari:

  • Simba inakwenda katika mchezo wa Jumapili ikiwa na lengo la kulinda rekodi yake ya ushindi iliyopata msimu uliopita ili kutimiza lengo lake la kutetea ubingwa

Dar es Salaam. Mabingwa wa Ligi Kuu Bara, Simba wameendelea na mazoezi kwenye Uwanja wa Gymkhana asubuhi hii.

Kocha wa Simba, Patrick Aussems ameanza kuwapa mazoezi mepesi wachezaji wake kwa kukumbia uwanja mzima kwa kasi ya kawaida.

Baada ya kumaliza mazoezi hayo walifanya ya viungo chini ya Adel Zrane ambayo yalikuwa ndani ya dakika 10.

Baada ya kumaliza mazoezi ya viungo kocha Aussems alipanga koni kisha kuwagawa wachezaji katika makundi mbalimbali.

Aussems aliwagawa wachezaji katika makundi kutokana na sehemu ambazo wanacheza.

Mabeki wa kati, kulia na kushoto viungo wa kukaba na kushambulia mawinga wa kushoto na kulia sambamba na mastraika.

Mazoezi hayo yalikuwa na lengo kwa kila mchezaji kufanya kazi yake kama ni kukaba, kupiga krosi au pasi.

Wakati huo mastraika ndio walikuwa sehemu ya mwisho na kazi yao ilikuwa ni kufunga tu.