Simba yasaka stamina ufukweni-VIDEO

Muktasari:

  • Mara ya mwisho Simba kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu ilikuwa na mwaka 2012.

Simba imeendelea na mikakati yake ya kujiimarisha kwa ajili ya Ligi Kuu na Kombe la Mapinduzi baada ya leo kufanya mazoezi ufukweni.

Mazoezi hayo yaliyoanza saa 2.00 asubuhi hadi 4.00 asubuhi yalisimamiwa na kocha msaidizi Masoud Djuma na Meneja Robert Richard.

Hata hivyo kundi kubwa la wachezaji wa kikosi chake halikuhudhuria kutokana na wengi kuwa kwenye majukumu ya timu za taifa na wengine mapumziko.

Djuma alisema kwa sasa msisitizo wao ni mazoezi ya kuwaweka fiti wachezaji na baada ya hapo wataingia kwenye ufundi.

"Tunataka hadi ligi itakapoendelea, wachezaji wawe katika hali nzuri kwa sababu hatutopata tena nafasi ya mapumziko marefu," alisema Djuma