Simbu awaza mkwanja London Marathon

Saturday November 11 2017

 

By Imani Makongoro

Dar es Salaam. Bingwa mara mbili wa Jumuiya ya Madola, Gidamis Shahanga amemtaka mwanariadha Alphonce Simbu kuthamini uzalendo kwanza na sio fedha!

Shahanga picha yake imewahi kutumika kwenye stamp ambazo zilikuwa kama malipo ya kusafirishia vifurushi enzi hizo na sasa amegeukia kumchambua mwanariadha Simbu.

Mkongwe huyo amefunguka baada ya Simbu kutoshiriki michezo ya madola ya Australia kwa kuwa tu ana mbio nyingine ya mwaliko za London marathoni.

Hata hivyo, awali Simbu aliweka bayana kwamba mbio za Madola na London zote zinafanyika Aprili lakini hivyo atalazimika kutoshiriki mojawapo.

Advertisement