Sinema ya Kelvin Yondani yahamia Yanga

Muktasari:

  • Taarifa kutoka kwa mmoja wa Wanayanga kwenye kundi maarufu la klabu hiyo amesema Tarimba atafanya kazi ya kuhakikisha anamalizana na Yondani na Kessy ambao wamebaki Dar es Salaam wakati kikosi hicho kikipaa Nairobi kuifuata Gor Mahia.

Mwenyekiti wa zamani wa Yanga, Abbas Tarimba ameamua kulichukua suala la kuhakikisha Kelvin Yondani na Hassan Kessy wanacheza tena Yanga msimu ujao.

Taarifa kutoka kwa mmoja wa Wanayanga kwenye kundi maarufu la klabu hiyo amesema Tarimba atafanya kazi ya kuhakikisha anamalizana na Yondani na Kessy ambao wamebaki Dar es Salaam wakati kikosi hicho kikipaa Nairobi kuifuata Gor Mahia.

Awali, kulikuwa na taarifa kwamba, Beki  huyo wa Yanga, Yondani wakati wowote anaweza kujiunga na Simba kwa uhamisho wenye thamani ya Sh 80milioni.

Yondani hakuambatana na Yanga kwenda Nairobi kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Gor Mahi utakaochezwa leo kwenye Uwanja Kasarani, Kenya.

Taarifa ilizozipata MCL Digital zilidai kuwa Yondani angekutana na viongozi wa Simba kuhusu kumsajili na kuna uwekezano kwenda kuonana na Mohammed Dewji 'MO'.

Chanzo hicho kimedai kuwa beki huyo Yondani ametaka kupewa Sh 80 milioni ili kusaini mkataba wa kujiunga na Simba.