Stand United yaigeukia Simba

Muktasari:

  • Stand United ilipata ushindi wake wa kwanza msimu huu kwa kuichapa Mbeya City mabao 2-1 na kujinasua kutoka mkiani hadi nafasi ya 12 kwenye msimamo wa ligi.

Kipa wa Stand United, Frank Muhonge amesema ushindi walioupata dhidi ya Mbeya City umewafanya wajiamini zaidi wanapokwenda kuikabili Simba Jumapili ijayo.

Stand United ilipata ushindi wake wa kwanza msimu huu kwa kuichapa Mbeya City mabao 2-1 na kujinasua kutoka mkiani hadi nafasi ya 12 kwenye msimamo wa ligi.

Muhonge alisema  wataongeza nguvu zaidi ili washinde mchezo ujao dhidi ya Simba kwani ushindi walioupata dhidi ya Mbeya City umewaongezea morali na kujiamini.

"Tunashukuru kupata ushindi wetu wa kwanza ambao umerejesha morali ndani ya timu na kutupa kujiamini kwa ajili ya michezo mingine ijayo ukiwemo dhidi ya Simba".

"Ushindi huo umetupa nguvu ya kupambana zaidi na naamini utatufanya kuwa moto katika michezo yote iliyo mbele yetu," alisema Muhonge.