Swaswea City yaiduwaza Liverpool

Muktasari:

  • Swansea City imeifunga Liverpool bao 1-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu England uliochezwa jana Jumatatu usiku.

England. Bao pekee la Alfie Mawson limeiwezesha Swansea City kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi Liverpool kwenye mchezo wa Ligi Kuu England uliochezwa jana Jumatatu usiku.

Ushindi wa Liverpool wiki iliyopita wa mabao 4-3 dhidi ya Manchester City uliwafanya kuingia uwanjani kwa kujiamini jambo lililowafanya kupoteza mchezo huo.

Swansea walistahili kupata ushindi huo kutokana na kuonyesha mchezo mzuri. Timu hiyo imepoteza mechi 19 walizocheza kwenye mashindano yote, hivyo bao la  Mawsom limefuta mkosi kwa kuipatia bao la ushindi.

Ushindi wa Swansea kwenye Uwanja wa Libert umewapa matumaini kushinda mechi zake zinazofuata itakapokutana na vigogo wengine wa EPL.