Tegete, Luhende wafunga usajili Kagera

Mwanza. Kagera Sugar imesema haina mpango wa kuongeza mchezaji baada ya kunasa saini za nyota saba wapya. Miongoni mwa wachezaji saba waliotua Kagera Sugar ni Jerry Tegete wa Majimaji na beki wa kushoto David Luhende kutoka Mwadui. Kocha msaidizi Ally Jangalu aliwataja wengine Amad Waziri, Hemed Khoja, Majid Khamis na Omari Mponda. Alisema Kagera imefunga hesabu za usajili kwa ajili ya msimu ujao.

(Saddam Sadick)