Timu ya Taifa ya Ngumi yajiweka mkao wa kula

Muktasari:

  • Kocha wa timu hiyo, David Yomba alisema wanaendelea vizuri na mazoezi ila wanaomba sapoti kutoka serikalini na wadau.

Dar es Salaam. Kikosi cha timu ya Taifa ya ngumi wakiwa wanaendelea na mazoezi ya kujiandaa na mashindano ya Jumuiya ya Madola.

Kocha wa timu hiyo, David Yomba alisema wanaendelea vizuri na mazoezi ila wanaomba sapoti kutoka serikalini na wadau.

"Kikosi kinaendelea na mazoezi na kabla ya kwenda kwenye mashindano mwisho wa mwezi huu, tutacheza mechi ya kirafiki na timu ya Ngome JKT," alisema Yomba.