Tottenham yajiweka ‘top four’ England

Muktasari:

  • Tottenham imekuwa ikiutumia vyema uwanja wake wa nyumbani wa Wembley.

 Klabu ya Tottenham imeendelea kujiimarisha kwenye msimamo wa Ligi Kuu England baada ya kuifunga Brighton mabao 2-0 kwenye mchezo wa EPL uliofanyika jana Jumatano usiku.

Mabao ya Tottenham yaliwekwa wavuni na Serge Aurier na Heung Min Son na kuwafanya Brighton kumaliza siku vibaya.

Mabao hayo mawili yameipandisha Spurs hadi nafasi ya nne na kuifanya kufikisha pointi 31 sawa na Liverpool na Burnley lakini ikiwa juu kutokana na tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.