VIDEO: Simba ya Uturuki yagombea uwanja wa mazoezi na Lyon

Muktasari:

  • Vurugu hizo zilianza wakati kocha wa viungo wa Simba, alipokuwa akiitoa mpira iliyowekwa uwanja na meneja wa African Lyon, Salehe Mkere.

Dar es Salaam. Mabingwa wa Ligi Kuu, Simba na klabu ya African Lyon zimeingia katika malumbano wakigombea uwanja wa mazoezi leo kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Vurugu hizo zilianza wakati kocha wa viungo wa Simba, alipokuwa akiitoa mpira iliyowekwa uwanja na meneja wa African Lyon, Salehe Mkere.

Kitendo kile kiliwatibua Lyon na kujikuta wakianza kuzozana na wenzao wa Simba huku kocha mkuu wa Simba, Mbelgiji Partick Assuems akiacha mazoezi na kwenda kuamulia majibizano ya Meneja wake na mtunza vifaa wa Lyon.

Simba ilitakiwa kumaliza mazoezi yake saa 4:30, lakini hadi saa 5:10 walikuwa wakiendelea na mazoezi wakati ukiwa ni muda wa African Lyon.

"Meneja wa uwanja alituruhusu kuwatoa Simba tangu muda huo kwani tayari muda wao ulishakwisha, wakatuomba wamalizie hadi saa 5:00 tukakubali.

"Ilipofika saa 5:10 nikamsikia  meneja wa Simba anamwambia kocha wake wasitoke waendelee tu akidhani mimi (mtunza vifaa wa Lyon) sijui kiingereza, kitendo kile hakikuwa kizuri ndiyo sababu tukajikuta tukitoleana maneno," alisema Mkere mtunza vifaa huyo wa Lyon.

Hata hivyo, Simba walilazimika kucheza nusu uwanja kwa dakika kama 20 kisha wakamaliza mazoezi ikiwa ni baada ya wachezaji wa Lyon nao kuingia uwanjani.