Van Gaal amshambulia Mourinho soka la kichovu

Muktasari:

Amsifu Guardiola kwa kutunza heshima yake klabuni hapo tangu alipojiunga miaka miwili iliyopita

England. Kocha wa zamani wa Manchester United, Louis van Gaal amemshambulia Jose Mourinho kutokana na kukiongoza kikosi chake juzi Jumapili jambo lililowafanya waonyeshe soka la kichovu na kufungwa na Manchester City.

Kocha huyo mwenye mika 66 amemvaa bosi huyo wa Manchester United kwa madai kwamba mtindo wake wa kucheza ndio umemponza.

Van Gaan ameweka wazi kwamba soka la kocha huyo ni kwamba linaboa uwanjani jambo ambalo liliwapa wapinzani wao kuwaadhibu kwa mabao 2-1.

Pia hakusita kumpa sifa kocha Pep Guardiola pamoja na safu yao ya ushambuliaji ambayo imekuwa makini kuzuia maadui.