Vigogo Yanga waongeza nguvu Moro

Muktasari:

  • Mabosi hao wakiongozwa na Mwenyekiti wa kamati ya usajili, Hussein Nyika pamoja na Mjumbe wake, Salum Mkemi, walifika  mpaka uwanja wa Highland kuangalia mazoezi ya timu yao.

Morogoro. Vigogo wa klabu ya Yanga kuamua kuweka kambi ya siku moja mjini Morogoro kwa lengo la kuweka sawa mikakati ya timu yao kufanya vizuri katika mchezo wa Jumapili dhidi ya Simba.

Mabosi hao wakiongozwa na Mwenyekiti wa kamati ya usajili, Hussein Nyika pamoja na Mjumbe wake, Salum Mkemi, walifika  mpaka uwanja wa Highland kuangalia mazoezi ya timu yao.

Nyika alisema kuwepo wao Morogoro kumewaongezea motisha wachezaji wake baada ya kuzungumza  mawili matatu kabla ya mchezo.

"Hatukuja huku tangu walivuoweka kambi, uwepo wetu huu  ni mzuri na tumewapa   motisha kuelekea mchezo huu lakimi hatuwezi kuweka wazi kwasasa," alisema.

Wakati huohuo; Wachezaji Ibrahim Ajib, Amis Tambwe, Andrew Vincent  na Thabaan Kamusoko walikosekana katika mchezo wa kimataifa, wamejiunga na wenzao mkoani hapa kwaajili ya maandalizi dhidi ya watami wao wa jadi Simba utakaopigwa Aprili 29.

 

Katika mazoezi hayo yaliyokuwa yanasimamiwa na Kocha Noel Mwandila pamoja na Shadrack Nsajigwa, walionekana kuwa wakali muda wote huku wakiwataka wachezaji hao kutekeleza yale waliyohitaji.