#WC2018 Fainali za Kombe la Dunia zaingia siku ya sita leo

Fainali za Kombe la Dunia zimeingia siku ya sita leo Jumanne baada ya timu mwenyeji Rusia kufungua mashindano hayo Juni 14 kwa kuitandika Saudia Arabia mabao 5-0.

Mchezo wa England dhidi ya Tuniasi umehitimishwa jana usiku na mabao mawili ya Harry Kane na kuifanya England kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Mechi zingine za leo zinawakutanisha Colombia dhidi ya Japan, nao Senegal watawavaa Poland.

Mchezo utakaofuata wa Russia watakutana na Misri hapo baadaye katika ngwe ya pili ya fainali hizo Kundi A.

Kikosi cha England kitacheza mechi yake  pili dhidi ya Panama Nizhny Novgorod siku ya Jumapili.

Fuatilia tovuti yetu ya Mwanaspoti kupata matukio mbalimbali pia na kwenye mitandao yetu ya kijamii kujua kila kinachojiri ndani na nje ya uwanja.