Wabaya wa Yanga hawa hapa

Thursday November 9 2017

 

By Gift Macha

KIUNGO Mghana wa Simba, James Kotei ameeleza kuwa mafanikio ya timu yao kuongoza Ligi Kuu Bara mpaka sasa umechangiwa kwa kiasi kikubwa na ushapu nyota wao wawili, Emmanuel Okwi na Shiza Kichuya.

Okwi na Kichuya ndio mastaa wa Simba kwa msimu huu wakiwa wamefunga mabao 13 kwa pamoja, sawa na asilimia 61 ya mabao yote ya Simba kwa msimu huu.

Kotei ambaye mkataba wake na Simba unamalizika mwaka 2019, alisema kasi ya mabao ya nyota hao wawili imekuwa msingi mkubwa kwao kufanya vizuri kwani wamekua na mchango mkubwa katika kila mchezo wanaocheza.

 

Advertisement