VIDEO: Wabongo waenda na mchele kuishabikia Stars Lesotho

Muktasari:

  • Msafara huo unatarajiwa kutua Lesotho, Ijumaa usiku tayari kwa mechi ya Jumapili.

Mashabiki wa timu ya Taifa 'Taifa Stars wameamua kununua kilo 60 za mchele kwenda nazo Lesotho kwa ajili ya matumizi ya chakula katika kipindi chote cha safari yao huko.

Mchele huo ulinunuliwa kwenye eneo la Chimala wakati msafara huo uliposimama kwa muda kwa ajili ya mapumziko mafupi.

Mashabiki hao walinunua mchele huo ambao watakuwa wanajipikia wenyewe kutokana na fedha walizochanga wakiwa safarini kiasi cha Shilingi 10,000 kila mmoja ambazo zilikabidhiwa kwa shabiki mwezao Silvester Haule ambaye pia ni mgombea ujumbe wa kamati ya utendaji ya Yanga.