Wajumbe Fifa wanunua bidhaa za utamaduni

Muktasari:

  • Wajumbe wa mkutano wa mkuu wa Fifa kwa mara ya kwanza wamekuja Tanzania kupanga ajenda za mkutano mkuu wa Juni nchini Russia

Dar es Salaam. Wajumbe wa mkutano wa siku moja wa FIFA jana wamekuwa kivutio wakichangamkia bidhaa za Masai kwa Wamasaidi.

Bidhaa hizo za utamaduni wa kimasai ni kutoka Ngorongoro mkoa wa Manyara walioletwa hapo Mahsusi Kwa mkutano huo kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere.

Hata hivyo, changamoto ya kuuza ilikuwa fedha kwani wengine walikuwa na dola na wengine kadi hawana fedha taslimu na kingine ni wamasai hao kutokuwa na chenji.

Baadhi ya bidhaa hizo ni shanga, hereni zilizotengenezwa kwa shanga, mapambo ya shingoni na bangili za mkononi na miguuni.

Baada ya kuchangamkia bidhaa hizo, wajumbe waliingia kwenye mkutano huo ambao utafanyika na kumalizika leoleo na baadhi ya wajumbe wataondoka kuendelea na majukumu mengine ya shirikisho hilo.