Wanachama waliomchagua Mo wazawadiwa Simba

Muktasari:

  • Manara amesema haikuwa kazi rahisi kwao kuupitisha mfumo huo na wanachama wakatulia na kumaliza zoezi hilo salama bila ya migogoro.

AFISA Habari wa Simba, Haji Manara amewapongeza wanachama na mashabiki wa klabu hiyo kwa kuchagua viongozi na kupitisha muundo mpya wa hisa chini ya muwekezaji wao, Mohammed Dewji 'MO'.

Akizungumza Dar es Salaam leo Jumatano  alisema haikuwa kazi rahisi kwao kuupitisha mfumo huo na wanachama wakatulia na kumaliza zoezi hilo salama bila ya migogoro.

Alisema sasa anatambua kuwa wanachama wanafahamu thamani ya timu yao, ukubwa na wameonyesha kuelewa nini maana ya uwekezaji katika klabu yao.

"Wanachama na wapenzi wa Simba kwa pamoja wanastahili pongezi na nilitegemea hilo kutoka kwa watu tofauti nje klabu yetu kwa hiki walichokifanya wanachama lakini hakijafanyika acha unitumie fulsa hii kuwapongeza," alisema Manara.