Watanzania wakusanyana kujazana uwanjani Lesotho

Muktasari:

  • wapo Stars ikiibuka na ushindi dhidi ya Lesotho itafuzu fainali za AFCON kwa mara ya pili baada ya kufanya hivyo mwaka 1980.

Watanzania kutoka maeneo mbalimbali nje na ndani ya nchi ya Lesotho wameanza kukusanyika kwenye hoteli ya Avani jijini Maseru saa chache kabla ya mchezo wa Taifa Stars dhidi ya Lesotho.

Mchezo huo unatarajiwa kuanza mnamo saa 10 jioni kwa saa za Lesotho ikiwa ni saa 11 jioni kwa saa za Tanzania.

Kundi hilo la Watanzania ambao wameanza kukusanyika katika Hoteli hiyo ni wale wanaoishi Lesotho na Afrika Kusini sambamba na wale waliosafiri kutoka Tanzania kuja hapa kwa usafiri wa basi na wengine ndege.

Stars inahitaji ushindi kwenye mchezo wa leo ili ifikishe pointi nane zitakazoifanya ifuzu moja kwa moja kwenye fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) mwakani.