Wenger apangua kikosi kabla kuivaa Atletico

Muktasari:

Wenger amesema langoni atamsimamisha David Ospina pamoja na kuwa haamini sana langoni.

London, England. Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger ametangaza saprize moja kali kabla ya mchezo wa Ligi Europa dhidi ya Atletico Madrid leo usiku.

Wenger amesema langoni atamsimamisha David Ospina pamoja na kuwa haamini sana langoni.

The Gunners inakwaana na kikosi cha Diego Simeone kwenye Uwanja wa Emirates, wakiwa na lengo moja kutwaa ubingwa wa Europa ili kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya kama ilivokuwa kwa Manchester United.

Licha ya umuhimu wa mchezo wenyewe, The Mirror liliripoti kwamba Wenger alisema hawezi kumpanga langoni kipa, Petr Cech katika kikosi cha kwanza licha ya kuwa fiti kwa mchezo huo baada ya kuwa majeruhi.

Cech hakucheza mechi waliyoshinda mabao 4-1 dhidi ya West Ham na aliumia nyonga kiasi cha kumtioa shaka katika mchezo na Atletico.

Wenger aliwashangaza wachezaji wake baada ya kupanga listi akisema, langoni atasimama Ospina, ambaye amecheza mechi nane tu za michuano hiyo.

Uamuzi wa Wenger umewashangaza wachezaji wa Arsenal kumpanga Ospina kwa kuwa hakuwa akicheza kila siku kikosini Arsenal kwa msimu mzima na Wenger anataka kuweka rehani heshima yake Ligi ya Europa.

Mesut Ozil hakuwemo kwenye kikosi cha West Ham tangu Wenger atangaze kuachaa na Arsenal mwisho wa msimu, na atareje kwenye kikosi cha Atletico.