Yanga FC uso kwa uso na Reha FC leo

Muktasari:

  • Yanga itawakosa nyota wake mahili ambao wapo kambini na Stars nchini Afrika Kusini kujindaa na mchezo wa kimataifa wa kufuzu AFCON 2019

Dar es Salaam. Kikosi cha Yanga kitacheza na Reha FC ya daraja la kwanza katika mchezo wa kirafiki leo Jumatano  saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Uhuru.

Yanga inacheza mchezo huo wa kirafiki ikiwa ni mechi ya pili kipindi hiki cha  mapumziko ya klabu za Ligi Kuu kupisha michezo ya kimataifa ya kufuzu AFCON 2019.

Viingilio katika mechi hiyo vimetangazwa kuwa VIP ni Sh5,000 huku jukwaa la mzunguko ikiwa Sh3,000.

Uongozi wa klabu hiyo umewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi ili kushuhudia mchezo huo ikiwa ni pamoja na kuwapa sapoti wachezaji.

Yanga ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na alama 26 sawa na watani zao Simba waliopo nafasi ya pili lakini wakitofautiana mabao.

Yanga itawakosa nyota wake mahili ambao wapo kambini na Stars nchini Afrika Kusini kujindaa na mchezo wa kimataifa wa kufuzu AFCON 2019.