Yanga Princes yatwaa ubingwa, yapanda Ligi Kuu

Muktasari:

  • Timu ya Yanga Princes, imetwaa ubingwa katika mashindano ya Ligi Daraja la Kwanza Wanawake baada ya kuichapa Tanzanite ya Arusha mabao 2-1, katika mchezo wa fainali. Mabao ya Yanga Mabao yote mawili ya Yanga yalifungwa na Tabea Aidan aliyekuwa nyota wa mchezo.

Dar es Salaam. Timu ya Yanga Princes imetwaa ubingwa wa Ligi Daraja la Kwanza Wanawake na kupanda Ligi Kuu, baada ya kuilaza Tanzanite ya Arusha mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam jana.

Mabao yote mawili ya Yanga yalifungwa na Tabea Aidan aliyekuwa nyota wa mchezo. Bao la Tanzanite lilifungwa na Agnes Pallangyo.

Kocha Yanga Princes, Maalim Saleh alisema wameanza mchakato wa kusajili wachezaji hodari kujiandaa na mashindano hayo."Tuna mpango wa kuwaacha wachezaji 10 na kusajili wengine 10 ambao tunaweza kuwachukua katika timu yoyote ikiwemo Simba,” alisema mshambuliaji huyo wa zamani wa Yanga.